Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa trichinosis/trichinellosis ni ugonjwa unaosababishwa na minyoo mviringo ambayo mabuu yake (trichinae) yanasafiri na kuingia kwenye misuli na kutengeneza uvimbe.

Sababu ya ugonjwa wa trichinosis/trichinellosis

Trichinella spiralis

Epidemiolojia ya ugonjwa wa trichinosis/trichinellosis

Unapatikana ulimwengini kote, lakini unapatikana kwa wingi sehemu nyingine na kwa uchache sehemu nyingine, kulingana na jinsi watu wanvyoandaa nakula nyama ya nguruwe au nyama mwitu.

Uambukizo wa ugonjwa wa trichinosis/trichinellosis

Kwa kula nyama mbichi au ambayo haijapikwa vizuri yenye mabuu, hasa nyama ya nguruwe na bidhaa za nyama ya nguruwe.

Muda kabla dalili kuanza

Dalili huanza siku 8-15 baada ya kula nyama yenye maambukizi

Nani yuko hatarini zaidi

Watu wote wako hatarini. Baada ya kuambukizwa unabakia na kinga ya muda mfupiUgonjwa wa trichinosis/trichinellosis

Dalili za ugonjwa wa trichinosis/trichinellosis

Kama mabuu yatasafiri na kuingia kwenye tishu zingine (ukiaachilia mbali misuli), yanaweza kusababisha;

Utambuzi wa ugonjwa wa trichinosis/trichinellosis

  • Historia ya kula nyama mbichi ya nguruwe au ambayo haijapikwa vizuri
  • Kuangalia mabuu (larvae) kwenye misuli baada ya kuchukua sampuli – muscle biopsy
  • Kipimo cha damu – serologic test

Matibabu ya ugonjwa wa trichinosis/trichinellosis

  1. Kulazwa kwa mgonjwa
  2. Mebendazole AU
  3. Albendazole AU
  4. Thiabendazole
  5. Kiwango kikubwa cha corticosteroid kwa siku 1-2 kikifuatiwa na kiwango kidogo cha dozi kwa siku kadhaa au wiki.

Kuzuia

  1. Elimisha jamii kuhusu umuhimu wa kupika vizuri nyama ya nguruwe na bidhaa zinazotokana na nyama ya nguruwe au nyama ya mwitu
  2. Kugandisha nyama ya nguruwe na bidhaa zake kunaua mabuu (trichinae)

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000631.htm#:~:text=Trichinosis

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *