Maelezo ya jumla
Ugonjwa wa trichomoniasis ni ugonjwa unaowapata wengi na ni mgumu kutibu unaosababishwa na protozoa wanaoishi kwenye via vya uzazi
Sababu ya ugonjwa wa trichomoniasis
Trichomonas vaginalis
Epidemiolojia ya ugonjwa wa trichomoniasis
Umesambaa dunia nzima, uko katika mabara yote na unawapata watu wa rangi zote, hasa watu wazima, unawapata zaidi wanawake wenye umri kati ya miaka 16 -35. Kwa ujumla, 20% ya wanawake wanapata ugonnjwa huu katika maiha yao.
Uambukizo wacugonjwa wa trichomoniasis
Kwa kukutana na majimaji kutoka ukeni au uchafu kutoka kwenye uume wa mtu aliyeathirika wakati wa ngono. Unaweza kuupta pia kwa kuchangia nguo za ndani zenye maambukizi.
Muda mpaka dalili kuanza
Ski 4-20, kawaida ni siku 7. Watu wengi wanaweza kubaki bila dalili zozote kwa miaka mingi na wanaendelea kuambukiza wengine.
Muda wa uambukizo wa ugonjwa wa trichomoniasis
Mtu anaweza kuendelea kuambukiza wengne katika kipindi chote cha maambukizi, inaweza kuwa miaka.
Nani yuko kwenye hatari
Watu wote wapo kwenye hatari, lakini ugonjwa/dalili zinaoneka zaidi kwa wanawake
Dalili za ugonjwa wa trichomoniasis
- Wanaume wengi wanabaki bila dalili, japo wengine wanaweza kuvimba maungio, na wachache kuvimba tezi dume au korodani (epididymitis)
- Maambukizi kwa wanawake kwa kawaida yana dalili
- Uchafu wenye harufu wenye rangi ya njano
- Wekundu wa uke, maumivu wakati wa kukojoa, kuwashwa au kukojoa mara nyingi (kwa 30-50 ya visa) na maumivu wakati wa ngono
- Dalili hizi kama uonavyo, haziitofautishi Trichomoniasis na maambukizi mengine
Utambuzi wa ugonjwa wa trichomoniasis
- Kwa kuchunguza majimaji ya uke kwa kutumia darubini unaweza kuona wadudu aina ya Trichomonas vaginalis wakizungukazunguka kwenye sampuli – wet mount
- Kupandikiza sampuli – culture – inachukua siku 3-7 kupata majibu
Matibabu ya ugonjwa wa trichomoniasis
- Metronidazole AU
- Clotrimazole vaginal suppository kwa wanawake wajawazito inatibu mpaka 50%
Kuzuia
- Fanya utambuzi na tibu wagonjwa
- Matumizi ya kondomu
- Elimisha jamii ili utafute matibabu wakati wanapohisi kuna uchafu unatoka sehemu za siri na wajizuie kushiriki ngono mpaka uchunguzi na matibabu ya wao na wenzi yamekamilika