Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa ukoma ni ugonjwa sugu unaosababishwa na bakteria na unaathiri ngozi, mishipa ya fahama na kwa wagonjwa wenye hali kali, inaweza kuathiri njia ya hewa.

Sababu ya ugonjwa wa ukoma

Mycobacterium leprae

Epidemiolojia ya ukoma

Japo unapatikana katika maeneo ya vijijini katika maeneo ya kitropiki, hali ya kiuchumi na kijamii ni muhimu zaidi katika kutokea kwake kuliko hali ya hewa. Ugonjwa wa ukoma unapatikana zaidi kusini mwa Asia, Maeneo ya kitropiki Afrika na Amerika ya kusini.

Uambukizo wa ugonjwa wa ukoma

Haifahamiki vizuri. Makazi na kukaa na mgonjwa kwa muda mrefu inachangia kuambukizwa. Mamilioni ya bakteria wanatolewa kwenye majimaji yanayotoka puani mwa mtu mwenye ugonjwa mkali. Vidonda kwenye ngozi vya wagonjwa ukoma vinaweza kutoa bakteria wengi. Yawezekana bakteria hawa waningia mwilini kupitia kwenye mfumo wa hewa na vidonda kwenye ngozi. Kwa watoto wenye umri chini ya mmoja, maambukizi hudhaniwa kuwa yametokea akiwa tumboni mwa mama – transplacental

Muda kabla dalili kuonekana

Miezi 9 mpaka miaka 20

Muda wa uambukizo wa ugonjwa wa ukoma

Mara nyingi uwezo wa kuambukiza wengine unaisha baada ya matibabu ya mfululizo kwa muda wa miezi 3, kwa kutumia dawa aina ya dapsone au clofazamin au ndani ya siku 3 baada ya kutumia rifampicin.

Nani yuko kwenye hatari ya kupata ukoma

Ili kupata ugonjwa wa ukoma inategemea sana uwezo wa mtu mwenyewe kutengeneza kinga dhidi ya maaambukizi haya. Kama kinga yako iko vzr hauwezi kupata ugonjwa

Dalili za ugonjwa wa ukoma

Dalili mara nyingi zinatofautiana kulingana na ukali wa ugonjwa mtu anaoupata kutegemea na kinga ya mwili aliyoweza kutengeneza. kuna ukoma hafifu (Paucibacillary) na ukoma mkali (Multibacillary)Ugonjwa wa ukoma

  1. Ukoma hafifu (PB); Ukoma wenye vimelea vichache. hii ni aina ya ukoma unaowapata watu wenye kinga kubwa dhidi ya ukoma. ukoma huu una vimelea vichache sana na mgonjwa mwenye aina hii ya ukoma haambukizi ugonjwa wa ukoma. Aina hii ya ukoma ina mabaka machache yasiyozidi 5
    • Baka au mabaka yasiyo na hisia, yenye rangi ya shaba na hutokea sehemu yoyote ya mwili. baka au mabaka yanaweza kuwa bapa au yaliyovimba, hayawashi na hukosa hisia ya mguso
    • Kuvimba au kuuma kwa mishipa ya fahamu ya mikono, uso na miguu na shingoni.
  1. Ukoma mkali (MB); ukoma wenye vimelea vingi. Hii ni aina ya ukoma unaowapta watu wenye kinga ndogo dhidi ya ukoma. Ukoma huu una vimelea vingi na mgonjwa mwenye aina hii ya ukoma huambukiza ugonjwa wa ukoma kama hajapata matibabu. Ukoma huu mkali una mabaka zaidi ya matano pamoja na dalili nyingine zote za ukoma.
    • Mabaka zaidi ya matano na kuvimba au kuuma kwa mishipa ya fahamu
    • Kuvimba vinundu kwenye masikio na shemu nyingine ya mwili
    • Ganzi kwenye mikono au miguu au vyote
    • Kuwepo kwa vidonda visivyouma mikononi na miguuni
    • Kushindwa kufumba jicho au macho
    • Kuishiwa nguvu kwa misuli na kukakamaa kwa viganja vya mikono na miguu
    • Kuvimba mwili kukiambatana na homa kali
    • Kupoteza baadhi ya viungo vya mwili kama vile vidole vya miguu au mikono
    • Kuwa na upofu

Utambuzi wa ugonjwa wa ukoma

  • Kufanya uchunguzi wa mwili – kuangalia mabaka kama yana hisia, kuvimba mishipa ya fahamu, vinundu n.k
  • Kuchuguza sampuli ya ngozi iliokwanguliwa kutoka eneo liloathirika -AFB
  • Sampuli ya ngozi ya sehemu iliyoathirika inatakiwa kuchukuliwa na kupelekwa kwa pathologist kwa utambuzi

Matibabu ya ugonjwa wa ukoma

  1. Dapsone + Rifampicin + cifazami
    • Tiba ya miezi 6- Kwa wagonjwa wa ukoma hafifu – Wanaona na daktari kila mwezi
    • Tiba ya miezi 12 – Kwa wagonjwa wa ukoma mkali- Wanaona na daktari kila mwezi
  1. Aspirin inatumika wanapopata shida na uvimbe mkali
  2. Kuna wakati watapata shida kubwa ya kuvimba na wanaweza kuhitaji dawa za kupunguza uvimbe aina ya corticosteroids

Vyanzo

https://medlineplus.gov/genetics/condition/leprosy/

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *