Ujauzito kutungwa nje ya mji wa mimba ina maana gani?

Ujauzito kutungwa nje ya mji wa mimba ni pale mtoto anapotungwa na kupandikizwa katika sehemu tofauti mwilini. Katika ujauzito wa kawaida, mtoto anapandikizwa na kukua kwenye mji wa mimba (uterasi). Ujauzito unapotungwa nje ya mji wa mimba, mtoto anapandikizwa na kukua nje ya mji wa mimba, hali ambayo ni hatari. Ni muhimu kutambua ujauzito uliotungwa nje ya mji wa mimba kabla haujasababisha madhara makubwa.

Nani anaweza kupata tatizo la ujauzito kutungwa nje ya mji wa mimba? 

Mtu yeyote anaweza kupata tatizo la ujauzito kutunga nje ya mji wa mimba. Uko kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la ujauzito kutunga nje ya mji wa mimba kama una umri kati ya miaka 35 na 44 na umeshawahi kupata maambukizi au kufanyiwa upasuaji katika maeneo ya nyonga (ndani ya mwili wako, chini ya kitovu). Kama unavuta sigara au unapata shida kupata ujauzito, uko kwenye hatari zaidi pia ya kupata tatizo la ujauzito kutungwa nje ya mji wa mimba.

Nitajuaje kama ujauzito nilio nao umetungwa nje ya mji wa mimba?

Kama una tatizo la ujauzito kutungwa nje ya mji wa mimba, utakuwa na dalili kama za ujauzito wa kawaida (hautapata damu ya hedhi, matiti yakuwa yanauma, mchafuko wa tumbo). Unaweza pia usiwe na dalili yoyote ile. Dalili nyingine za ujauzito uliotungwa nje ya mji wa mimba ni maumivu na kutokwa damu ukeni. Unaweza pia kuhisi maumivu makali kama umechomwa na kisu tumboni au kwenye upande mmoja wa mfupa wa nyonga. Kama ukivuja damu sana, unaweza kujihisi kizunguzungu na hata kuzimia/kupoteza fahamu. Daktari anaweza kufanya kipimo ili kuhakikisha kama unauzito umetungwa nje ya mji wa mimba.

Nifanye ni nini kama nina tatizo la kutungwa kwa mimba nje ya mji wa mimba?

Daktari anaweza kukupatia dawa ili kuuzuia ujauzito kuendelea kukua au unaweza kuhitaji kufanyiwa upasuaji.

Je, nitapata tena tatizo la ujauzito kutungwa nje ya mji wa mimba nikipata mimba tena?

Kama umeshawahi kuwa na tatizo la ujauzito kutungwa nje ya mji wa mimba, uko kwenye hatari zaidi ya kupata mwingine nje ya mji wa mimba. Unaweza pia kupata shida sana kupata ujauzito mwingine. Unapaswa kujipatia muda ili kupona kabla ya kuanza kujaribu kupata mtoto mwingine baada ya ujauzito uliotungwa nje ya mji wa mimba

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ectopicpregnancy.html

Shares:
2 Comments
  • Seth
    Seth
    May 25, 2022 at 6:18 am

    Mwanamke anapo ingia hedhini japo ana uja uzito kati ya wiki 1 mpaka mwezi,na baada ya hapo zinakata,anakuwa na tatizo gani.

    Reply
    • Dr Mniko
      Dr Mniko
      May 29, 2022 at 11:32 pm

      ni vizuri akamwona daktari afanyiwe uchunguzi

      Ila baadhi ya wanawake wanapata matone ya damu kama ya hedhi mimba inapojipandikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba, hili huwa linatokea kuanzia siku 8 mpaka 10. baada ya hapo hatapata hedhi tena

      Ni vzr akafika kwa daktari kwa msaada zaidi

      Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *