Ngozi

Sio rahisi kujua mtu anaweza kuishi kwa muda gani bila ngozi.

Siku 2 ni makadrio mazuri, ila bado hatuna uhakika.

Ngozi, kucha na nywele hufanya kazi ya kukinga viungo vya mwili dhidi ya mazingira yanayouzunguka.

Ngozi ndio kiungo kikubwa zaidi kuliko vyote kwenye mwili.

Ngozi inasaidia kufyonza virutubisho, kudhibiti joto la mwili na kuondoa uchafu mwilini.

Tabaka la juu kabisa la ngozi ‘’Epidermis’’ ni mstari wa kwanza wa ulinzi.

Dermis ni tabaka la ngozi lililo katikati.

Lina mishipa ya fahamu inayokusaidia kuhisi unapoguswa.

Tezi za jasho zinapunguza joto la mwili kwa kutoa jasho mwilini

Tezi za sebaceous zinatengeneza mafuta ambayo husaidia hulainisha ngozi na kukukinga na maambukizi ya bakteria.

Mishipa ya damu na limfu inayopatikana kwenye tabaka la kati, huiletea ngozi virutubisho vyote inayohitaji.

Ngozi inahitaji kutunzwa.

  • Usikae sana kwenye jua,
  • kunywa maji ya kutosha,
  • chagua bidhaa za ngozi kwa umakini,
  • kagua ngozi mara kwa mara kama kuna mabadiliko.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/imagepages/19679.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *