Maelezo ya jumla

Ukiziwi ni hali ya kushindwa kusikia vizuri au kushindwa kabisa kusikia sauti kwenye sikio moja au yote mawili.

Je, ni zipi dalili za ukiziwi?

Dalili za ukiziwi ni pamoja na:

  • Baadhi ya sauti zinaweza kusikika kwa nguvu sana na zikakuumiza
  • Unaweza kupata shida kufuatilia maongezi hasa ya watu wawili au zaidi wanapozungumza
  • Kupata shida kusikia kwenye eneo lenye makelele
  • Kushinda kutambua na kutofutisha sauti za juu (kama vile “ s “ au “ th “)
  • Unapata shida kusikia sauti za wanawake kuliko za wanaume
  • Unapata shida kusikia kama kuna kelele mahala ulipo
  • Unasikia sauti kama vile unanong’onezwa (unasikia sauti kwa mbaliii)

Dalili nyingine ni kama vile:

Ni nini husababisha ukiziwi?

Zifuatazo ni sababu za ukiziwi”

  • Ukiziwi unaotokana na kuharibika kwa muundo wa sikio sehemu ya nje au sehemu ya ndani unaitwa kitaalamu – conductive hearing loss.
    • Kuharibika kwa vimfupa vitatu vilivyo ndani ya sikio ambavyo hufanya kazi ya kusafirisha sauti kutoka kwenye ngoma ya sikio kwenda ndani. Kama vimfupa hivi “ossicles” vikiharibika unaweza kuwa kiziwi
    • AU kama ngoma ya sikio kwa sababu yoyote ile haitetemi vizuri inapopigwa na sauti
      • Matatizo yanayosababisha ukiziwi unaotokana na kuharibika kwa muundo wa sikio mara nyingi yanatibika. Baadhi yao ni pamoja na:
        • Kujaa kwa nta ndani ya sikio
        • Kuharibiwa kwa vimfupa vidogo vinavyosafirisha sauti kutoka kwenye ngoma ya sikio
        • Kujaa kwa maji ndani ya sikio baada ya maambukizi ya sikio
        • Kukwama kwa kitu ndani ya sikio
        • Kutoboka kwa ngoma ya sikio
        • Kutokea kwa kovu kwenye ngoma ya sikio kwa sababu ya maambukizi ya mara kwa mara
  • Ukiziwi unaotokana na kuharibika kwa mfumo wa neva unaopokea sauti na kuipeleka kwenye ubongo, aina hii inaitwa sensorineural hearing loss. Aina hii ya ukiziwi inayotokana na kuharibka kwa mishipa ya fahamu ni ngumu kuitibu, na mara nyingi haitibiki kabisa.
      • Ukiziwi unaotokana na kuharibika kwa mfumo wa neva wa kusikia unasababishwa na:
        • Uvimbe wa “ acoustic neuroma” – huu ni uvimbe kwenye neva/ mshipa wa fahamu unaobeba taarifa kutoka kwenye sikio kwenda kwenye ubongo
        • Ukiziwi unaohusiana na umri
        • Maambukizi utotoni, maambukizi kama vile homa ya uti wa mgongo, matubwitubwi na surua
        • Ugonjwa wa meniere’s – ugonjwa huu unasababisha mtu kujihisi kuanguka na kizunguzungu
        • Kukaa au kufanya kazi maeneo yenye kelele nyingi sana
        • Kutumia baadhi ya dawa
  • Ukiziwi unaweza kuwepo baada ya kuzaliwa ( wa kuzaliwa nao) na aina hii inaweza kusababishwa na:
    • Kutofautiana kwa shinikizo la hewa nje na ndani ya ngoma ya sikio – hasa kwa waogeleaji wanaozama kwenda kima cha chini cha bahari – scuba diving
    • Kuvunjika kwa fuvu (kunaweza kusababisha kuharibika kwa muundo wa sikio na neva/ mishipa ya fahamu inayotumika katika kusikia)
    • Majeraha yanayotokana na milipuko, kurindima kwa risasi, mziki uliowekwa kwa sauti kubwa na earphones

Utambuzi wa tatizo la ukiziwi

Daktari atachukua historia yako ya kimatibabu na kufanya uchunguzi wa mwili.

Baadhi ya vipimo vinavyoweza kufanyika ni pamoja na:

  • Audiometry – hiki ni kipimo kinachosaidia kutambua ni aina gani ya ukiziwi na kwa kiasi gani huwezi kusikia
  • Picha ya CT au MRI scan ya kichwa – vipimo hivi hufnyika ili kuangalia kama kuna uvimbe au mvunjiko kwenye mifupa ya fuvu au ubongo
  • Tympanometry – kipimo hiki kinaangalia mitetemo ya ngoma ya sikio

Ni wakati gani unapaswa kuomba msaada haraka?

Ongea na daktari kama:

  • Ukiziwi au kupungua kwa uwezo wa kusikia kunaanza kuathiri mfumo wako wa Maisha
  • Kama ukiziwi au tatizo la kushindwa kusikia haliondoki au linazidi kuwa baya zaidi
  • Kama uwezo wa kusikia umepungua sana kwenye sikio moja kuliko jingine
  • Kama una ukiziwi ulitokea haraka sana na kwa ghafla au kama unasikia kelele kwenye masikio
  • Kama una dalili nyingine pia, kama vile, maumivu ya sikio, pamoja na matatizo mengine ya kusikia
  • Kama unapatwa na maumivu ya kichwa ambayo hayakuwepo zamani, unajihisi uchovu au kama unapata ganzi sehemu yoyote ya mwili.

Uchaguzi wa matibabu

Baadhi ya mambo unayoweza kufanya nyumbani:

  • Unaweza kuondoa nta kwenye masikio polepole kwa kutumia bomba la sindano na maji ya uvuguvugu. Unaweza pia kununua dawa maalumu ya kulainisha nta ya masikio (kama vile cerumenex) ili iweze kutoka.
  • Kuwa makini unapokuwa unatoa vitu vilivyokwama kwenye masikio. Kama kitu kichokwama kwenye sikio kinaleta shida kutolewa ni bora kwenda kwa mtaalamu wa afya akitoe. Usitumie vifaa vyenye ncha kali kutoa kitu sikioni. Onana na daktari mapema kama unahisi uwezo wa kusikia umepungua.
  • Baadhi ya aina hizi za upasuaji zinaweza kuboresha usikivu kwa baadhi ya watu wenye ukiziwi.
    • Kurekebisha ngoma ya sikio
    • Kuweka vimrija vidogo kwenye ngoma ya sikio ili kuondoa majimaji yaliyojaa nyuma ya ngoma ya sikio baada ya maambukizi
    • Kurekebisha vimfupa vidogo vilivyo nyuma ya ngoma ya sikio – ossiculoplasty
  • Baadhi ya yafuatayo yanaweza kusaidia kwa mtu ambaye atabaki na ukiziwi kwa mda mrefu:
    • Kupatiwa vifaa vitavyomsaidia kusikia vizuri
    • Kujifunza njia mbalimbali zitazokusaidia kuwasiliana na wengine
    • Kujifunza lugha ya alama (kwa wale wenye ukiziwi mkali sana)

Baadhi ya watu wanafanyiwa upasuaji wa kupandikiziwa kufaa ndani ya sikio ili kisaidie kusikia – cochlear implant – aina hii ya tiba inafanyika kwa watu ambao hali yao ni kali kiasi kwamba vifaa vya kusaidia kusikia havisaidii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/hearingdisordersanddeafness.html

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *