Maelezo ya jumla

Kama kidole cha mguu kinauma, ni chekundu na kimevimba kuzunguka ukucha, kuna uwezekano mkubwa utakuwa umesababishwa na ukucha unaokua kwenda ndani ya ngozi au nyama. Kwa sehemu kubwa vidole gumba vya miguu ndio huwa vinaathirika zaidi. Ukucha unaanza kukua kuelekea ndani ya ngozi kwa pande zote mbili na kwa sababu hiyo eneo hilo linavimba. Wakati mwingine, sehemu iliyovimba inapata maambukizi na unaweza kuona usaha unatokea hapo. sababu kuu ya tatizo hili ni kukata kucha vibaya au kuvaa viatu ambavyo vinabana na kukaza vidole vya miguu.

Kama una ukucha unaokua kwenda ndani ya ngozi akati gani umwone daktari

Panga kumwona daktari kama:

  • Ukucha umevimba na unaonekana una maambukizi
  • Una ugonjwa wa kisukari au ugonjwa mwingine wowote unaosababisha mzunguko wa damu kwenye miguu kupungua

Unachoweza kufanya mwenyewe ukiwa nyumbaniukucha unaokua kwenda ndani ya ngozi

Kwenye hatua za mwanzo, unapoona kidole  cha mguu kimevimba kiasi, unaweza kujitibu wewe mwenyewe ukiwa nyumbani kwa kufauta utaratibu ufuatao. Ukifanya mambo yafuatayo yanaweza kutosha kabisa kuhakikisha tatizo haliwi kubwa zaidi

  • Loweka mguu mara mbili kwa siku kwa dakika 10 kwenye maji ya uvuguvugu ndani ya bakuli, maji hayo yawe yametiwa vijiko 2-3 vya chumvi. Baada ya hapo chukua kitambaa safi kilichokaushwa juani na ufunike eneo hilo au nunua ”gauze” ufunge. Ni vizuri kuvaa viatu vya wazi wakati kama huu.
  • Usikate ukucha mpaka utakapoona umepona kabisa
  • Usijaribu kupaka rangi ya kucha au kujaribu kuondoa rangi uliyokuwa umeipaka wakati kidole kikiwa kimevimba

Kuzuia ukucha unaokua kwenda ndani ya ngozi

Njia nzuri ya kuzuia kucha za miguuni kukua kuelekea ndani ya ngozi ni kutunza vizuri miguu yetu

  • Osha miguu vizuri kila siku na uikaushe vizuri
  • Usivae viatu ambavyo vinakubana au kukandamiza vidole. Ni vizuri kuepuka viatu ambavyo vimechongoka kwa mbele au vyenye kisigino kirefu
  • Badili soksi mara kwa mra, tafuta soksi za pamba. Kama unatumia ”pantyhose” au ”tights”, nunua ambazo hazifuniki miguu au nunua za pamba na zibadili mara kwa mara.
  • Kata kucha vizuri

Namna nzuri ya kukata kucha

Unaweza kuanza kutumia njia hii unapokuwa unakata kucha, itasaidia kuzuia kucha za miguu kuota kwenda ndani. Kama wewe ni mzee au kama una kisukari au kama una matatizo ya kuona, omba ushauri kwa mtaalamu ili akuoneshe jinsi ya kutunza kucha.

  • Lainisha kucha kabla ya kuzikata kwa kuzilowesha kwa muda wa dakika 10 kwenye maji ya uvuguvugu yaliyowekwa kwenye bakuli au baada ya kuoga. hii itasababisha ziwe rahisi kukata, hasa kama una kucha ambazo ni ngumu
  • Tumia mkasi wa kukatia kucha au kikata kucha ”clippers” ili kuzikata vizuri. Zikate kwa mzunguko na uzifanye kama za duara kwenye sehemu ya juu, lakini usikate kwenye ncha au kona za kucha, ukifanya hivi unazichochea kukua kuelekea ndani ya ngozi. Baada ya hapo sawazisha ukucha wako kwa kuusugua taratibu
  • Kama utaona kuwa ukucha wa kidole cha mguu umeanza kuota kuelekea ndani ya nyama au ngozi, usijaribu kuuchimbua au kuukata ua kujaribu kusukuma kitu chochote chini yake

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001237.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *