Maelezo ya jumla
Bhangi ndiyo mhadarati unaotumiwa vibaya zaidi kati ya vijana duniani. Vijana hutumia bangi kwa sababu nyingi. Huenda waitumie kwa vile wana tamaa ya kujua inavyohisi, kufanana na wenzao au kuwa wa kisasa, au huenda wasukumwe kuitumia na vijana wenzao. Vijana pia wanaweza kutumia bangi ili kukabiliana na hofu, hasira, mfadhaiko, au uchovu.
Bhangi ni mchanganyiko wenye rangi ya kijani kibichi, kahawia au kijivu, wa majani, mizizi, mbegu na maua ya mmea yaliyokaushwa, kukatakatwa. Majina ya kawaida ya bangi ni kama: Msuba, ganja, majani, cha Arusha, cannabis, weed, grass, pot, hash, au hashish.
Bhangi huvutwa kwa kuisokota iwe kama sigara (inayoitwa joint) au huvutwa kwenye kiko. Mtu anapovuta bangi, yeye huhisi athari yake karibu papo hapo, na wao huchukuliwa kuwa “wamelewa.” Kulewa huku husababishwa na kemikali fulani iliyo kwenye bhangi inayoitwa THC, inayoathiri ubongo na sehemu zingine za mwili. Kuna athari nyingi za muda mfupi na mrefu za uvutaji bangi.
Athari za Muda Mfupi za bhangi
Katika muda mfupi, matumizi ya bhangi yanaweza kusababisha matatizo yafuatayo mwilini:
- Hisia nzito ya furaha (kulewa)
- Ugumu kuzingatia na kuwa makini
- Kufanya maamuzi yasiyo ya kawaida
- Kufanya maamuzi ya pupa bila kufikiria
- Kukosa motisha
- Matatizo ya kumbukumbu/fahamu
- Macho mekundu
- Midomo iliyokauka
- Hamu kubwa ya kula – unakula sana
- Mapigo ya moyo yaliyoongezeka
- Hofu, woga, kutoamini watu, au kushuku watu
- Matatizo ya usingizi
- Majeraha yasiyokusudiwa; kama yanayotokana na ajali ya gari
Athari za Muda Mrefu za bhangi
Uvutaji bangi kila wakati au kwa muda mrefu huweza kusababisha matatizo yafuatayo mwilini:
- Shida za kupumua
- Kiwango pungufu cha uerevu (IQ)
- Athari mbaya kwa masomo
- Kutoridhika na maisha
- Mfadhaiko/Ugonjwa wa sonona
- Hofu
- Fikra za kujiua
- Shida nyingi za kifamilia, mahusiano kuvunjika
Kweli zingine kuhusu bangi unazopaswa kujua.
Bhangi inasababisha kufeli shuleni. Utumiaji banghi unaweza kuwa na athari mbaya, na kusababisha kupungua kwa umakini, kumbukumbu/ufahamu, na uwezo wa kujisomea kwa siku au wiki kadhaa—hasa unapoitumia kila wakati. Vijana wavutao bangi hupata alama za chini sana na huwa na uwezekano mkubwa wa kuacha masomo kuliko vijana wasiovuta bhangi. Utumiaji bangi unaweza kupunguza uerevu/IQ yako ukiivuta kila wakati katika miaka ya ujana. Watumiaji bhangi kwa muda mrefu huripoti kuridhika kidogo katika maisha yao, matatizo ya kumbukumbu/ufahamu na shida za kimahusiano, afya mbovu ya kimwili na kiakili, mishahara midogo, na fanaka mdogo kitaaluma/kikazi.
Kwa vile bangi huathiri uamuzi, inaweza kuhatarisha maisha ya watu. Bhangi, sawa na dawa zingine zinazotumiwa vibaya, inaweza kutatiza uamuzi. Hii huweza kusababisha tabia zenye hatari ambazo zinaweza kumweka mtumiaji kwenye hatari ya kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi.
Ni hatari kuendesha gari baada ya kutumia bangi. Bangi huathiri ustadi unaohitajika kwa uendeshaji salama—umakini, uangalifu, na uwezo wa kuitikia matukio ya kwa wakati. Bhangi hutatiza uwezo wa kutambua umbali kati ya kitu kimoja na kingine na hupunguza uwezo wa kujibu isha au sauti anapokuwa barabarani. Ukiachilia mbali ulevi wa pombe, bangi ndio mhadarati unaochangia ajali nyingi zaidi barabarani, ikiwemo zile zinazosababisha vifo.
Unaweza kutawaliwa/uraibu wa bhangi. Siyo kila mtu avutae bhangi hutawaliwa. Hata hivyo, utumiaji bangi kila wakati huweza kusababisha kutawaliwa. Hii inamaanisha kuwa mtu hawezi kuacha kutumia bangi ingawa angependa kuacha.
Bangi inachukuliwa kuwa “mhadarati-mfunguzi.” Watumiaji wa bangi wana uwezekano mkubwa wa kujaribu, mihadarati inayodhuru afya zaidi katika siku za usoni.
Vyanzo
https://medlineplus.gov/marijuana.html