Je, unyanyasaji wa nyumbani ni nini?
Unyanyasaji wa nyumbani (home violence) pia huitwa ukatili majumbani. Ukatili ni neno linaloelezea mtu anayefanya jambo ili kumuumiza au kumtisha mtu mwingine mara kwa mara. Huu ukatili hujumuisha kuumiza mwili wa mtu, kuumiza hisia zake, au kumfanya afanye mambo ambayo yanamfanya ajihisi vibaya au ambayo hataki kufanya. Ukatili pia huhusisha kujaribu kumfanya mtu ajihisi kuwa yeye si mwerevu au mjasiri, au hawezi kufanya uamuzi kuhusu maisha yake mwenyewe
Je, ni nani anayeweza kunyanyaswa nyumbani?
Mtu yeyote anaweza kunyanyaswa nyumbani, watu wazima, watoto na hata wazee. Katika familia ambapo ukatili inafanyika, wanawake, watoto, na wazee ndio huumia zaidi.
Watoto wanaoshuhudia ukatili nyumbani huwa waoga na wenye huzuni mwingi. Mara nyingi, watoto hawa huamini kuwa tabia zao au wao wenyewe ndiyo chanzo cha migogoro hiyo. Si vizuri kiafya, kimwili na kiakili kwa watoto kuishi katika nyumba yenye ukatili wa aina hii. Watoto wanaoshuhudia mzozo au migogoro nyumbani mara kwa mara huwa na matatizo shuleni, huanza kutumia madawa ya kulevya na pombe na wanaweza kuwa wajeuri.
Je, utajuaje kama unanyanyaswa?
Unadhulumiwa ikiwa mtu katika nyumba yako:
- anakusukuma, anakupiga kofi au ngumi,
- anakutishia kukuua au kukuumiza,
- anakutishia kuwachukua watoto wako,
- anakukosoa na kukuaibisha kila wakati,
- hakuruhusu uone familia na marafiki zako,
- anakulazimisha kufanya ngono wakati hautaki,
- hakuruhusu kufanya kazi na upate pesa zako,
- hakuruhusu ujifunze Kiingereza au kujifunza kuendesha gari,
- anakutishia kukurudisha nchi yako, na
- anachukua hati zako za uhamiaji
Unyanyasaji wa nyumbani ni uhalifu
Unyanyapaa wa majumbani haupaswi kuwekwa siri. Unyanyasaji wa kimwili au kingono dhidi ya mtu wa familia ni kinyume cha sheria nchini Tanzania. Polisi na korti huwalinda waathiriwa wote wa unyanyasaji. Mtu ambaye ni mjeuri nyumbani anaweza kukamatwa na kufungwa jela.
Ikiwa unanyanyaswa, haimaanishi kwamba wewe si mke au mama mzuri. Mtu ambaye anakudhulumu anataka kutawala maisha yako.
Ikiwa kuna mtu katika familia yako ambaye anakudhulumu, unapaswa kujua kwamba hauko peke yako. Ikiwa unamjua mtu ambaye anadhulumiwa, wajulishe kwamba kuna usaidizi unaopatikana
Nini cha kufanya kama unadhulumiwa
Mtu katika nyumba yako akikuumiza wewe au watoto wako, ni muhimu kwamba utafute usaidizi:
- Zungumza na mtu unayemwamini: rafiki, jirani, mtu wa familia, au mwanasheria kuhusu shauri lako
- Fika kituo cha polisi ili kutoa taarifa ili upate usaidizi
Ukweli ni kuwa uamuzi wa kuzungumza unaweza kuwa mgumu sana, kunaweza kuwepo na sababu nyingi sana za kukufanya usizungumze kabisa, lakini jipe ujasiri. Yawezekana hali yako ikaboreka zaidi baada ya kuzungumza na kupata usaidizi