Upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili ni nini?
Upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili hupunguza ukubwa wa tumbo na kulifanya liwe dogo na kubadili homoni zinazopeleka taarifa za njaa. Kuna aina kuu tatu za upasuaji zinazopendelewa zaidi nazo ni kufunga sehemu ya tumbo (gastric banding), kukata sehemu ya tumbo (sleeve gastrectomy) na njia ya kutengeneza mfuko wa chakula kama mbadala wa tumbo (roux-en-Y gastric bypass). Lengo la aina hizi za upasuaji ni kumfanya mtu ahisi ameshiba baada ya kula chakula kidogo, kwa hiyo unakula kidogo na kupunguza uzito.
Upasuaji wa kupunguza uzito kwa kufunga tumbo ni nini?
Upasuaji huu unahusisha kutumia kifungio cha silicone kubana na kufunga sehemu ya juu ya tumbo ili kulipunguza ukubwa. Tumbo likisha fungwa inakula chakula kidogo na kujihisi umeshiba. Daktari anaweza kusogeza kifungio ili kuongeza au kupunguza ukubwa wa tumbo ili kudhibiti kupungua kwa uzito
Upasuaji wa kupunguzaa uzito kwa kukata sehemu ya tumbo na kuliondoa ni nini?
Sehemu ya tumbo inakatwa na kuondolewa, hii inasababisha kutengenezwa kiungo chenye muundo wa bomba na hivyo kupunguza ukubwa wake. Kwa sababu ukubwa wa tumbo umepungua, utakula chakula kidogo na kujihisi umekua. Homoni zinazoashiria kuwa una njaa pia zinapungua
Upasuaji wa kupunguza uzito kwa kutengeneza kimfuko kingine cha kutunzia?
Upasuaji huu unahusisha kutengeneza kimfuko kingine kidogo kitakachofanya kazi ya kutunzia chakula na kuvuka kabisa sehemu nyingine ya tumbo na sehemu ya utumbo. Baada ya upasuaji huu, kimfuko kilichotengenezwa ni kidogo, mwili unanyonya kiwango kidog0 zaidi cha kalori kutoka kwenye chakula, na homoni zinazoashiria kuwa una njaa zinapungua. Mabadiliko haya yanapelekea kupungua kwa uzito.
Nani anaweza kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito?
Watu wenye uwiano wa uzito na urefu (body mass index) zaidi ya 40, au watu wenye uwiano wa uzito na urefu (BMI) wa 35 na wana moja au zaidi ya matatizo ya kitabibu yanayotokana na uzito mkubwa, wanaruhusiwa kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito kama wameshindwa kupungua uzito kwa kutumia njia za kawaida.
Je, nitaweza kula vyakula va kawaida baada ya upasuaji wa kupunguza uzito ?
Kuna mpango wa chakula maalumu unaopaswa kuufuata baada ya upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili. Kamwe hautawahi kula kama ulivyokuwa ukila awali, na hautakuwa ukijihisi mwenye njaa kama ulivyokuwa ukihisi zamani. Njaa itapungua.
Je, bima inaweza kulipia upasuaji wa kupunguza uzito?
Ni vizuri kufuatilia kuhusu suala hii kwa mtoa bima wako kabla, bima nyingi zinalipia upasuaji wa kupunguza uzito, lakini kagua kwanza.
Angalizo
Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaii kuhus shida hii.