Mdomo na meno
Ni muhimu sana kutunza usafi wa mdomo na meno katika nchi za kitropiki. Kama usafi huu hautazingatiwa, mabaki ya chakula yaliyonasia kwenye meno huoza na kusababisha magonjwa ya fizi na meno na mdomo kunuka.
Ili kupunguza shida hii, ni vizuri kupiga mswaki na kusuuza mdomo kwa maji mengi baada tu ya kula. Maji ya kusuuza mdomo yanaweza kuwa ya kawaida au yaliyotiwa chumvi kidogo. Katika mazingira ambayo mswaki wa kawaida haupatikani, miswaki ya kienyeji kwa kutumia miswaki ya miti ambayo inafaa katika mazingira ya kijijini. Kama magonjwa ya fizi na kuoza kwa meno kutatokea, ni muhimu kumwona daktari ili tatizo lishughulikiwe.
Ni vizuri kuzuia watu kutumia vipande vya kioo au mkaa au viu vingine vigumu kuondoa au kukwangua sehemu ngumu ya nje ya jino (enamel).
Kichwa, pua na macho
Kkichwa
Kichwa na nywele kinapaswa kuwekwa safi kwa kunawa na maji na sabuni kila wiki. Kichwa kichafu kinaweza kutunza wadudu kama chawa, ambao wanaweza kusambaza magonjwa. Kukosa usingizi kwa sababu ya kuwashwa kunaweza kusababisha hali duni ya afya. Vumbi kwenye kichwa inaweza kuruhusu minyoo kukua.
Pua
Pua, ni sehemu ya mfumo wa kuvuta hewa, ina vinyweleo vinavyosafisha hewa na wadudu kutoka kwenye hewa inaopita. Kwa hiyo pua inatoa ulinzi kwa mapafu kwa kuzuia vitu vibaya kuingia. Ni kwa sababu hii, ni muhimu pua kuwa safi kwa kutumia kitambaa au kwa kupuliza pua ili kutoa uchafu na vumbi. Kwa njia hii, maambukizi yanayoanzia kwenye pua na koo yatadhibitiwa.
Macho
Mcho machafu yanapendwa na nzi. Kunawa macho mara kwa mara huacha macho safi. Vimelea wanaobebwa kwenye miguu ya nzi wanaweza kuwekwa kwenye macho na kusababisha upofu. Mfano wa ugonjwa unaosumbua wengi katika mazingira yetu ya vijijini ni ugonjwa wa trakoma. Ugonjwa wa trakoma unaweza kuzuiwa na kunawa mara kwa mara/
Unapaswa kuosha macho muda gani?
- Muda wa asubuhi unaponawa uso
- Baada ya kukutana na vumbi au vitu vingine vinavyosumbua macho
- Kama umeshika macho na mikono michafu
- Baada ya kukutana na moshi na masizi
- Maji unayotumia hakikisha hayana uchafu.
Jifunze zaidi hapa kuhusu kusafisha;
Vyanzo
https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/conditionsandtreatments/personal-hygiene