Maelezo ya jumla kuhusu usafi wa miguu
Usafi wa miguu – kwa wengi wetu tunasita kunawa miguu mara kwa mara ukilinganisha na mikono. Hii inaweza kuwa inatokana na kuiona miguu iko mbali au sio kiungo muhimu sana. Kwa sababu hatuzingatii kusafisha vizuri vidole vya miguu vinaweza kupata matatizo kadhaa ya afya. Katikati ya vidole, kutokwa jasho kunatengeneza mazingira mazuri ya fangasi kukua. Kama usafi wa vidole vya miguu usipozingatiwa, harufu mbaya inaweza kusababisha karaha hasa kama unafanya kazi kwenye ofisi isiyo na hea ya kutosha.
Katika jamii zinazoishi vijijini chini Tanzania, watu wantembea bila kuvaa viatu/peku. Watu wanoishi katika jamii hizi wanapaswa kunawa miguu mara nyingi zaidi kuliko wanaovaa viatu.
Kama mtu asipozingatia usafi wa mguu, minyoo na funza wanaweza kuingia na kusababisha maambukizi.
Namna ya kusafisha miguu (usafi wa miguu)
Unaweza kuiweka safi miguu kwa kusafisha:
- Miguu
- Viatu
- Soksi
Baada ya viatu na soksi kuoshwa vinapaswa kuwekwa juani ili kukauka na kuua vimelea. Vivyo hivyo, baada ya kunawa mikono, unapaswa kusubiri kwanza miguu ikauke kabla ya kuvaa viatu.
Njia ya kuzuia magonjwa ya miguu
- Nawa miguu kwa sabuni mara kwa mara
- Vaa soksi safi ili kunyonya jasho kama inawezekana
- Vaa viatu
Katika maeneo ya vijijini ambapo watu hawawezi kununua viatu ambavyo ni ghali, kutumia viatu vilivyotengenezwa kienyeji vinafaa. Shida ya fangasi inayotokana na kuvaa viatu vya ngozi, haipo kama utatumia viatu vya wazi vya kienyeji.
Jifunze zaidi hapa kuhusu kusafisha;
Vyanzo
https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/conditionsandtreatments/personal-hygiene