Maelezo ya jumla

Usafi wa ngozi – jasho na mafuta yanayotolewa yanasababisha uchafu kunatia kwenye ngozi. Hii inaziba matundu ya ngozi na kutatanisha utedaji kazi wake. Bakteria wanawez kuzaliana kwa haraka juu ya ngozi na kusababisha magonjwa na harufu mbaya. Baadhi ya aina za nzi wanaweza kuzalia mayai yao kwenye nguo zilizoanikwa nje kukauka na mtu akizivaa mabuu yanayotoka yanatotoa na kuingia ndani ya ngozi na kusababisha karaha. Kama vimelea na wadudu wanaoishi kwenye ngzoi kwa sababu ya usafi duni watasababisha kidonda, ulizi wa kuvilinda viungo vya ndani ya mwili unapotea na maambukizi yanaweza kusambaa mwili mzima.

Njia za kuhudumia ngozi (usafi wa ngozi)

  • Oga mwili kwa maji na sabuni angalau kila siku ili kuondoa vumbi na uchafu
  • Vaa nguo zinazokutosha na zinazofaa kulingana na hali ya hewa
  • Kukaa kwenye mwanga wa jua na hewa nzuri kunafaa

Usafi wa nguo

Nguo zinatukinga na baridi na matatizo mengine na kutuutia mwili joto. Nguo zilizochafu zinachangia kukua na kusambaza wadudu wanaoweza kusababisha magonjwa. Kuvaa nguo safi mcha na usiku ni muhimu sana kwa afya.

Jasho linalotoka kwenye miili yetu linajazana kwenye mwili. linaweza kusababisha harufu mbaya. Hata hivyo, ni vyema kuweka nguo katika hali ya usafi kama tunavyoitunza miili yetu. Nguo zinaweza kuoshwa kwa maji na sabuni au aina nyingine ya bidhaa inayotumika kiasili. Baada ya kuoshwa zinapaswa kukaushwa kikamilifu kwa jua/upepo. Eneo maalumu linapaswa kutafutwa au kutengwa kwa ajili ya kufulia ili kuzuia zisichafuliwe. Matatizo ya afya yanayotokana na nguo chafu ni pamoja na:

  • Ugonjwa wa homa ya typhus
  • Relapsing fever
  • Kunuka
  • Kuwashwa mwili, vidonda, n.k.

Ili kuzuia matatizo haya:

  • Fua na badili nguo mara kwa mara hasa za watoto kwa sababu zinachafuka kirahisi
  • Osha nguo mara kwa mara, zikaushe na ikiwezekana piga pasi na ziweke mahala pasafi
  • Osha matindo na nguo za kulalia mara kwa mara kama vile mashuka
  • Kuanika nje mara kwa mara nguo nzito kama blanketi na nyingine
  • Kuchemsha kwa dakika 10 au kuanika nje kwenye jua nguo zote zenye chawa
  • Kuua chawa kwa kutumia kemikali kama 10% DDT au 1% malathion na kuziacha kwa siku 1 wakti wa mlipuko wa chawa
  • Weka nguo zenye chawa kwenye mfuko wa plastiki na ufunge, kisha uweke kwenye jua mara kwa mara mpaka utakapoona chawa waliokufa. Hii inaweza kuchukua siku 2-3 au zaidi kutegemea na kiasi cha nguo na mwanga wa jua uliopo. Kwa mara nyingi, mfuko mweupe wa plastiki unapendelewa zaidi
  • Kama kuna mlipuko wa chawa, toa taarifa kwa mamlaka husika

Jifunze zaidi hapa kuhusu kusafisha;

Vyanzo

https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/conditionsandtreatments/personal-hygiene

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *