Vidonda kwenye sehemu za siri ni nini?

Vidonda kwenye sehemu za siri – kuna vidonda vinavyopatikana kwenye uume au uke au maeneo yanayozunguka. Kwa kawaida magonjwa yanayosababisha vidonda yanasambazwa kupitia uke, mdomo, au mkundu. Vidonda vinaweza pia kupatikana kwenye mkundu au kwenye ngozi inayouzunguka. Wakati mwingine, vidonda vinauma na vinatoa majimaji.

Ni nini husababisha vidonda kwenye sehemu za siri?

Vidonda kwenye sehemu za siri mara nyingi vinasababishwa na magonjwa ya ngono, hasa ugonjwa wa malengelenge (herpes), kwa mara chache kaswende, na kwa nadra sana ugonjwa wa pangusa/chancroid. Kwa wanaume wanaoshiriki ngono kinyume na maumbile, kaswende ndio ugonjwa unaowasababishia vidonda zaidi.

Vidonda vinaweza pia kusababishwa na magonjwa yanayosababisha uvimbe (uvimbe unapotokea kwa sababu ya mjibizo mbaya unaotokana na kinga ya mwili [kwa mfano, ugonjwa wa psoriasis, ugonjwa yabisi kavu, ugonjwa wa lupus]), jeraha, au mjibizo mbaya unaotokana na bidhaa za ngozi unazotumia.

  • Ugonjwa wa malengelenge – husababisha malengelenge mengi madogomadogo yanayouma yaliyojaa majimaji mepesi
  • Ugonjwa wa masundosundo – husababisha viuvimbe kama vinyama vinavyoota kwa mfano wa mkauliflawa
  • Ugonjwa wa pangusa – husababisha uvimbe karibu na sehemu za siri, na ndani ya siku moja hutumbuka kutengeneza kidonda
  • Ugonjwa wa kaswende – husababisha kidonda kidogo, usio na maumivu kabisa kwenye sehemu za siri
  • Granuloma inguinale – viuvimbe vidogo vyekundu vinatokea kuzunguka sehemu za siri na mkundu

Nani anaweza kupata vidonda kwenye sehemu za siri?

Mambo yanayoongeza hatari ya kupata vidonda kwenye sehemu za siri yanafanana na yale yanayoongeza hatari ya kupata magonjwa ya ngono. Yanahusisha kufanya ngono isiyo salama, kutokutahiriwa, na kuwa na wapenzi wengi. Vidonda kwenye sehemu za siri vinavyosababishwa na magonjwa yanayosababisha uvimbe vinaweza kuwa vya kurithi.

Nitawezaje kupunguza hatari ya kupata vidonda kwenye sehemu za siri?

Unaposhiriki ngono, tumia kondomu. Hii inapunguza hatari ya kupata, lakini unapaswa kukumbuka kuwa unaweza bado kupata vidonda kwenye sehemu za siri kupitia sehemu ya ngozi ambayo haijafunikwa na kondomu.

Nitajuaje kama nina vidonda kwenye sehemu za siri?

Vidonda kwenye sehemu za siri vinajitokeza kwa namna tofautitofauti. Vinaweza kuanza kama viuvimbe au kama upele na vinaweza vikawa vinauma au haviumi. Unaweza pia kuwa na tezi zilizovimba kwenye kinena (kuvimba mtoki) au homa. Daktari anaweza kukutibu kwa kuangalia tu vidonda vyako na kwa baadhi ya visa anaweza kuagiza vipimo ili kuangalia kama vinatokana na magonjwa ya ngono.

Vidonda kwenye sehemu za siri vinatibiwaje?

Matibabu ya vidonda kwenye sehemu za siri yanategemea sababu yake. Magonjwa ya ngono kwa kawaida hutibiwa kwa kutumia antibiotiki au sindano au vidonge vya kudhibiti virusi. Kama una ugonjwa unaosababisha uvimbe, unaweza kuhitaji sindano au mafuta ya kupaka kwenye kidonda. Baadhi ya vidonda kwenye sehemu za siri vinapona tu vyenyewe lakini vinaweza kuendelea na kusababisha maambukizi makali. Daktari atatibu maumivu uliyonayo, atashughulikia kidonda na kufanya vipimo vingine kama vinahitajika. Mwone daktari upate matibabu sahihi haraka.

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa na wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003221.htm

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *