Maelezo ya jumla

Vidonda vya homa / vidonda baridi / tukuto, huanza kwa kuwepo kwa mwasho karibu na midomo, kisha kunatokea mkusanyiko wa vipele vidogo ambavyo baada ya muda vinatengeneza malengelenge. Malengelenge haya yakishapasuka, yanatengeneza ganda kifuniko na baadae kwa kawaida kinapona baada ya siku 10. Tatizo hili huwa linasababishwa na kirusi anayeitwa ”herpes simplex virus” ambaye akiingia mwilini mara ya kwanza anajificha na hasababishi madhara. Lakini ukipata mafua, msongo, uchovu, hedhi, upepo, au kama umekaa kwenye jua kwa muda mrefu kunafanya virusi hawa kuamka na kusababisha vidonda mdomoni.

Mwone daktari kama

Mwone daktari mapema kama unaona unapata kidonda ndani au karibu na jicho

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Hauwezi kuwaondoa hawa virusi wanaosababisha vidonda vya homa, hakuna dawa inayoweza kuwaondoa kabisa, lakini unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza au kuongeza kasi ya vidonda kupona na kupunguza uwezekano wa kupata vingine mara kwa maravidonda vya homa

  • Unapoanza tu kuhisi midomo inaanza kuwashawasha, chukua pakiti ya barafu kisha uweke hapo (unaweza kuchukua barafu ikiwa kwenye mfuko wa plastiki ukaiweka kwenye kitambaa laini, kisha ukaiweka mahali palipoathirika), weka kwa angalau dakika 5-10 kila baada ya dakika 30
  • Tumia dawa za maumivu kama kidonda kinakupatia karaha sana. Madawa ya maumivu kama vile ‘’Acetaminophen’’ au ‘’ibuprofen’’ husaidia kupunguza karaha za kidonda cha homa
  • Paka mafuta kwenye eno lilioathirika ili kuepuka kupasuka na hata kutokwa damu kwa midomo
  • Vidonda vya homa vinaambukiza, unaweza kumuambukiza mwingine. Wakati ukiwa na kidonda epuka kubusiana na usichangie taulo, vikombe au nyembe na watu wengine
  • Baada ya kushika kidonda cha homa ni vizuri kunawa mikono ili kuepuka kusambaza virusi vyake. Usifinye, kukuna au kubonyeza kidonda
  • Kama unaenda kukaa sehemu yenye jua au upepo, paka vizuri midomo mafuta, yatasaidia kupunguza uwezekano wa kupasuka midomo
  • Kama msongo au uchovu ndio huwaamsha hawa virusi, hakiksha unalala vizuri au unaweza ukajifunza njia za upumuaji na ku-relax ili zikusaidie kudhibiti msongo. BONYEZA HAPA KUJIFUNZA NJIA HIZI
  • Kama unapata vidonda vya homa mara kwa mara daktari anaweza kushauri utumia ‘’Acyclovir cream’’. Dawa hii inatolewa na daktari na inadhibiti virusi wasiongezeke na kupunguza muda na ukali wa vidonda. Unapaswa kujipaka dawa hii mara tu unapoanza kuhisi mwasho kwenye midomo

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

  • Unaona kidonda au vidonda vinaendelea kukua au hali unaonainazidi kuwa mbaya zaidi au kama unaona hali haijaaa sawa baada ya siku 10 za matibabu
  • Unapata vidonda vya homa mara kwa mara

Vyanzo

https://medlineplus.gov/coldsores.html

Shares:
1 Comment
  • Anthony
    Anthony
    March 26, 2021 at 4:31 pm

    Hey! I know this is kinda off topic however I’d figured I’d ask.
    Would you be interested in trading links or maybe guest
    writing a blog post or vice-versa? My site discusses a lot of the
    same subjects as yours and I feel we could greatly benefit from each
    other. If you might be interested feel free to shoot me an e-mail.
    I look forward to hearing from you! Wonderful blog by the way!

    Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *