Maelezo ya jumla
Sio kwamba wanaopata ugonjwa wa masikio ‘’otitis externa’’ ni wanaoogelea pekee. Unapooga au kuosha nywele, unyevunyevu unaobakia kwenye masikio unaweza kuwa na vimelea ambao wakiingia sikioni wanaweza kusababisha maambukizi. Tatizo hili pia, linaweza kuwapata watuambaowanafanya kazi kwenye maeneo ya joto au yenye unyevuunyevu mwingi. Unapokuwa na ugonjwa huu, sikio linaweza kuwasha, kuwa na maumivu (hasa unapolishika au kulivuta) na unaweza kuhisi kama limeziba. Kunaweza pia kuwepo na uchafu au majimaji yanayotoka kwenye sikio lililoathirika.
Mambo yafuatayo yanaweza kusababisha usumbufu au harara na kusababisha maambukizi kwenye njia ya sikio:
- Kama umeikwaruza sehemu ya ndani ya njia ya sikio
- Kama umepata mjibizo mbaya ”allergy” unaotokana na mzio wa kemikali zilizo kwenye dawa ya matone ya kuweka kwenye sikio au kama umetumia dawa ya kubadili nywele na kwa bahati mbaya ikaingia kwenye sikio
Ukiwa na ugonjwa wa masikio, mwone daktari kama
Panga kumwona daktari kama unadhani una ugonjwa wa masikio unaowapata watu wanaoogelea ‘’swimmers ear’’ ili afanye utambuzi
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe kama una ugonjwa wa masikio
Kama ukishughulika na ugonjwa wa masikio mapema unakuwa umepona ndani ya wiki moja au mbili. Kuna mambo kadhaa unayoweza kufanya ili kujipunguzia karaha au unapoendelea kutumia matibabu uliyopewa na daktari
- Sikio litakuwa linawasha, lakini epuka kujikuna
- Usitumie dawa ya kudondoshea kwenye sikio ‘’eardrops’’ kama haujaelekezwa na daktari
- Ni muhimu kuhakikisha kuwa sikio halipati unyevu wakati wote wa matibabu na siku kadhaa baada ya matibabu. Oga badala ya kuogelea. Kama unataka kuosha nywele, hakikisha maji hayaingii kwenye masikio kwa kuziba njia ya sikio kwa pamba ambayo umeipaka mafuta ‘’petroleum jelly’’. Ziondoe pamba baada ya kumaliza kuosha nywele. Usiogelee mpaka maambukizi yatakapo kuwa yameondoka.
- Kama una maumivu kwenye sikio chukua chupa yenye maji ya moto kisha ishikilie kwenye sikio au chukua kitambaa kikavu kilichopaswa kwa moto au pasi ukishikilie kwenye sikio, itasaidia kupunguza maumivu. Au unaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu.
- Unaweza kutumia dawa kama ”Acetaminphen” au ”ibuprofen” ili kupunguza maumivu
- Kama unaona kuna majimaji ua uchafu unaotoka sikioni, weka pamba kwenye sehemu ya nje ya sikio ili ifyonze uchafu unaotoka. Hakikisha kuwa unabadisha mara kwa mara pamba uliyoiweka.
- Usijaribu kusafisha sikio kwa kutumia vijiti vya kusafishia masikio ‘’cotton swabs’’ wakati wa maambukizi ya sikio au wakati mwingine wowote. Vijiti hivi vinaweza kuharibu masikio.
Kuzuia tatizo hili
Kama unapata ugonjwa huu wa masikio mara kwa mara, fanya mambo yafuatayo, kujikinga:
- Kama una ogelea mara kwa mara, vaa ‘’earplugs’’ kwenye masikio. Vifaa hizi zitasaidia kuzuia maji yasiingie sikioni na kusababisha maambukizi. Epuka pia kuogelea kwenye maji machafu au yaliyochafuliwa.
- Hakikisha unakausha vizuri masikio baada ya kuogelea, kuosha nywele au baada ya kuoga. Egemeza kichwa kwenda upande mmoja, kisha ivute sehemu laini ya sikio ili kusaidia maji kutoka. Unaweza pia kutumia ‘’hair dryer’’ ili kukausha kwa ndani
- Tumia ”shampoo” zisizo na ”perfume” kali na epuka kutumia dawa ya kubadili rangi ya nywele na bidhaa za mitindo ya nywele.
Mwone daktari kama
Ni vizuri kupanga kumwona daktari kama:
- Dalili zinazidi kuwa mbaya zaidi au kama haujaona mabadiliko yoyote hata baada ya kufuatilia matibabu uliyopewa kwa siku mbili
I love your work and I would like to be part of the program but I live in Dodoma, can the program also start in Dodoma
hello, asante kwa kutuandkia
kwa sasa hatuna programme iliyopangwa Dodoma, ila shirika letu limesajiliwa kuhudumia Tanzania bara nzima, i hope one day tutafika na huko kufanya kazi.
kama ungependa kushiriki katika juhudi zetu za kuelimisha umma, unaweza kufanya hivyo kupitia tovuti hii, jiunge katika tovuti hii ili kutoa elimu ya afya kwa umma. unaweza kuandika makala na kisha kuiweka hapa kwa ajili ya jamii yako. Asante na karibu.